Jumatano 8 Julai 2026 - 15:00
Mazishi ya Imam Shahidi Khamenei ni Kuifanya Upya Ahadi ya Njia ya Heshima na Utukufu

Hawza/ Abu Alaa al-Wala'i, Katibu Mkuu wa Kata'ib Sayyid al-Shuhadaa, huku akisisitiza nafasi ya mashahidi katika Umma wa Kiislamu, amesema: "Kushiriki katika mazishi ya mashahidi si ibada ya kihisia pekee, bali ni kufanya upya ahadi kwa malengo ya Mwenyezi Mungu, njia ya Ahlul-Bayt (as) na maadili ya heshima na utukufu."

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa al-Wala'i, Katibu Mkuu wa Kata'ib Sayyid al-Shuhadaa, amesema katika ujumbe wa video akizungumzia tukio la kihistoria la mazishi ya mwili wa Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei nchini Iraq: "Leo tumesimama mbele ya tukio la kipekee; tukio ambalo limechanganya machozi na heshima, huzuni na fahari pamoja na uaminifu."

Aliongeza: "Leo tumekusanyika kuupokea na kuusindikiza mwili mtukufu wa kiongozi ambaye alisimama bega kwa bega na taifa la Iraq, na katika nyakati ngumu zaidi alitumia uwezo wake wote katika kutetea haki, heshima na utukufu."

Katibu Mkuu wa Kata'ib Sayyid al-Shuhadaa wa Iraq, akieleza kwamba; mazishi ya Imam Shahidi Ayatullah Khamenei si hafla ya hisia na majonzi pekee, alisisitiza: "Ushiriki huu ni ishara ya uaminifu kwa njia ya heshima na utukufu, na ni uthibitisho wa kuendelea na njia ya mashahidi pamoja na maadili ambayo walijitolea maisha yao kwa ajili yake."

Al-Wala'i pia alitoa wito kwa makundi mbalimbali ya wananchi, wanazuoni wa vyuo vikuu, maprofesa, vijana na wanaharakati wa kijamii kushiriki katika hafla hiyo, akisema: "Kushiriki katika mazishi ya mashahidi si kuusindikiza mwili pekee, bali ni kufanya upya ahadi kwa Mwenyezi Mungu na kwa njia ya Ahlul-Bayt (as)."

Aidha alibainisha: "Mataifa kamwe hayatawasahau wale waliojitolea kwa ajili ya heshima na utukufu wao."

Mwishoni, Katibu Mkuu wa Kata'ib Sayyid al-Shuhadaa wa Iraq alisisitiza: "Uaminifu wa kweli kati ya mataifa na viongozi haujengwi kwa maneno na kaulimbiu pekee, bali hupata maana kupitia ukweli, kujitolea na kusimama pamoja na wananchi."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha